Yanga - Local

Yanga vs Mtibwa Sugar, Azam Complex leo

Joel JJ By Joel JJ
16 Dec 2023
Yanga vs Mtibwa Sugar, Azam Complex leo

Burudani ya ligi kuu inaendelea uwanja wa Azam Complex leo wakati mabingwa watetezi Yanga watakapo wakaribisha Mtibwa Sugar katika mchezo utakaopigwa saa 12:30 jioni

Ni mchezo utakaozikutanisha timu zenye malengo tofauti, Yanga inahitaji ushindi ili kuisogelea Azam Fc ambayo iko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama nne ikiwa imecheza mechi tatu zaidi

Mtibwa Sugar wanaburuza mkia wakishinda mechi moja tu msimu huu lakini timu hiyo inanolewa na Kocha Zubeir Katwila ambaye Wananchi wanamkumbuka kwani ndiye kocha pekee aliyepata ushindi dhidi ya Yanga msimu huu wakati akiinoa Ihefu Fc

Kwa Kocha Miguel Gamondi, huu ni mchezo muhimu kwa kikosi chake kushinda ili kuongeza morali kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama Fc utakaopigwa Jumatano, Disemba 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwenye makaratasi unaweza kuonekana ni mchezo mwepesi kwa Yanga lakini kiuhalisia haitakuwa mechi nyepesi

Kwa ubora ambao Yanga wameonyesha kwenye ligi msimu huu, kila timu inapocheza na Yanga inatamani kuingia kwenye rekodi ya kufanikiwa kuwazuia Wananchi kuibuka na ushindi

Hivyo ni mechi ambayo kwa Mtibwa Sugar itakuwa kama fainali wakati Yanga wao watahitaji kuendeleza ubabe wao kwenye ligi msimu huu

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
7h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
8h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
10h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
10h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
11h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
11h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
11h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
12h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
12h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
14h ago
READ MORE →