Juventus inataka kumsajili kiungo wa kati Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips mwezi Januari, na nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anaripotiwa kuwa tayari kuhama. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)
Crystal Palace wameonyesha nia ya kumtaka mchezaji wa Arsenal na Uingereza Eddie Nketiah, 24, wakati wa dirisha la uhamisho la Januari. (Football Transfers)
Arsenal na Manchester City zote zinalenga kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 25, bila klabu yoyote kutishwa na thamani ya Aston Villa £100m. kwa mchezaji huyo(Football Insider)
Wawakilishi wa winga wa Uingereza Jadon Sancho wanajaribu kulazimisha uhamisho wa kuondoka Manchester United, kwa nyota huyo lakini makubaliano ya kubadilishana wachezaji kumhusisha wing'a huyo mwenye umri wa miaka 23 na Borussia Dortmund huenda yakawa na ugumu sana (Givemesport) (Givemesport)
Chelsea na Manchester City wameomba kufahamishwa kuhusu kiungo wa kati wa River Plate raia wa Argentina Claudio Echeverri, 17. (Fabrizio Romano)
Manchester United inataka kuwaondoa wachezaji msimu ujao ili kumsajili beki wa Real Madrid na Austria David Alaba, 31. (Fichajes kupitia Football Transfers)
Everton wana nia ya kumsajili mshambuliaji mwenye umri wa miaka 23 wa Marseille na Senegal Iliman Ndiaye.(Teamtalk)
Fulham wanafikiriakumsajili kiungo wa kati wa Feyenoord na Uholanzi Mats Wieffer mwenye umri wa miaka 24. (Football Insider)
Manchester City wanatarajiwa kuungana na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kupata sahihi ya nyota wa Girona mhispania Miguel Gutierrez mwenye umri wa miaka 22, (Manchester Evening News)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, mwenye umri wa miaka 28, pia yuko kwenye Orodha ya Juventus ya uhamisho ya uhamisho wao Januari(Tuttosport - kwa Kiitaliano)
BBC