Simba - Local

Simba yaifumua Wydad 2-0 CAF CL

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Dec 2023
Simba yaifumua Wydad 2-0 CAF CL

Mnyamaaaaaaaaaa amefanya yake uwanja wa Benjamin Mkapa akiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wydad Casablanca katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika

Huu ni ushindi wenye thamani kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi kwani umerejesha katika nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo

Zilikuwa dakika mbili za maajabu kutoka kwa Willy Essomba Onana akifunga mabao yote katika dakika ya 36 na 38

Alifunga bao la kwanza kwa shuti la nje kidogo ya 18 baada ya kutengewa pasi murua kutoka kwa Kibu Denis

Dakika mbili baadae Onana akawainua Wanamsimbazi kwa mara nyingine akiweka kambani bao bora la mchezo huo baada ya kupasiana 1-2 na Mzamiru Yassin

Kwa hakika leo Onana alikuwa na jambo lake kwani aliwapa wakari mgumu walinzi wa Wydad. Huyu ndiye Onana ambaye Wanamsimbazi walikuwa wakimsubiri tangu msimu huu ulipoanza

Alipata majeraha kwenye kipindi kocha Abdelhak Benchikha akilazimika kumtoa nafasi yake kuingia Israel Mwenda

Benchikha alifanya mabadiliko zaidi kwenye kipindi cha pili yaliyokuwa na lengo la kulinda ushindi

Duchu, Khamis, Bocco wote waliingia kuhakikisha alama zote tatu zinabaki Msimbazi

Simba imechupa mpaka nafasi ya pili ikifikisha alama tano, ikiwa bado na mecho moja nyumbani dhidi ya Jwaneng Galaxy

Kimahesabu Simba inahitaji alama tisa tu kutinga robo fainali kwa maana ushindi dhidi ya Jwaneng na angalau sare dhidi ya Asec katika mchezo unaofuata ambao utapigwa huko Ivory Coast mwezi Februari 2024

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’