Real Madrid wanakaribia kufanya hatua ya kushtukiza kumsajili mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 30, kutoka klabu ya Uturuki ya Galatasaray. (Marca)
Borussia Dortmund wanavutiwa na beki wa Tottenham Hotspur Mhispania Sergio Reguilon, 27, ambaye anaichezea Manchester United kwa mkopo. Reguilon ana kipengele cha kumaliza mkopo wake katika mkataba wake. (Bild - kwa Kijerumani, usajili unahitajika)
Brentford imezitahadharisha Arsenal na Chelsea kwamba watalazimika kulipa ada 'inayostahili' ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney, 27. (Talksport)
Tottenham, Aston Villa na Brighton wamefanya mawasiliano na Juventus kumhusu winga Muingereza Samuel Iling-Junior, 20, ingawa bado hakuna ofa yoyote iliyotolewa. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)
RB Leipzig wana nia ya kumsajili winga wa Manchester United Jadon Sancho, 23, lakini kumudu mshahara wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kunaweza kuwa tatizo kwa klabu hiyo ya Ujerumani. (Bild - kwa Kijerumani, usajili unahitajika)
Wakati Sancho anaweza kuondoka, Manchester United haitarajii kufanya usajili wowote mkubwa mwezi Januari, mkurugenzi wa soka John Murtough amewaambia mashabiki. (The Athletic)
Kiungo wa kati wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, hatalengwa tena na Liverpool mwezi Januari. Vilabu vingine vya juu vinamtaka , ingawaje, Bayern Munich wanamchukulia kuwa na gharama ghali sana. (Sky Sport Germany)
Newcastle United wameanza mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Lewis Miley, 17, kuhusu kusaini mkataba wa muda mrefu atakapofikisha miaka 18 baadaye msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Klabu ya Preston North End ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Dan Gore, 19, kwa mkopo kwa msimu uliosalia. (Manchester evening News)
Copenhagen iko tayari kumuuza winga wa Uswidi Roony Bardghji, 18, anayelengwa na Chelsea, Manchester United na Tottenham, mwezi Januari. (90 min)
BBC