Msuva apewa mkono wa kwaheri JS Kabylie

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th December 2023


Msuva apewa mkono wa kwaheri JS Kabylie

Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imechana na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva

Katika taarifa yake Kabylie mbali na Msuva pia imeacha na mshambu-liaji mwingine mkongwe Hichem Mokhtar raia wa Taifa hilo

Msuva aliyejiunga na klabu hiyo Agosti 27,2023 akitokea Al - Qadsi-ah ya Saudi Arabia hakufanikiwa kuwa mwanzo mzuti ndani ya timu hiyo kwa kukosa kuanza kwenye mechi nyingi na Waalgeria hao

Ujio wa kocha Mreno Lui Almeida umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa Msuva ndani ya Kybalie baada ya kocha huyo kushindwa kukubaliana na uwezo wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga

Almeida amewaambia mabosi wa Kabylie kuwa anataka washambuliaji wengine wawili wenye makali zaidi tofauti na hawa ambao a emewa-tema


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.