Juventus wamejadiliana na Manchester City kuhusu mkataba wa mkopo wa kiungo wa Uingereza Kalvin Phillips. (ESPN)
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameiambia Manchester City kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo mwezi ujao, huku Newcastle United pia ikiwa na nia ya kumnunua kwa mkopo. (Guardian)
Arsenal wanafikiria kutoa pauni milioni 52 kumnunua beki wa Sporting Lisbon na Ureno Goncalo Inacio, 22, mwezi Januari. (Sun)
Chelsea haitapokea ombi lolote kutoka kwa Tottenham la kutaka kumnunua kiungo wao wa kati Conor Gallagher, 23, katika uhamisho wa Januari licha ya kutokuwa na uhakika juu ya hali ya mkataba wake. (Football Insider)
Tosin Adarabioyo, 26, ameiambia Fulham kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu ujao kwa uhamisho wa bure. Beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana wa Uingereza amewahi kuzivutia Tottenham na Monaco. (Sun)
Tottenham wataelekza darubini yao kwa wachezaji wengine ikiwa hawataafikiana na beki wa Ufaransa na Nice Jean-Clair Todibo wiki chache zijazo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 pia amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United. (Teamtalk)
Rennes wako tayari kuachana na kiungo Nemanja Matic, 35, mwezi Januari. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Serbia alijiunga na klabu hiyo ya Ligue 1 kutoka Roma msimu uliopita. (L'Equipe)
Barcelona na Real Madrid wanaongoza katika mbio za kumsajili Mason Greenwood, 22, lakini Manchester United kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha Old Trafford muda wake wa mkopo katika klabu ya Getafe utakapomalizika. (Talk sport)
Winga wa Juventus na England aliye na umri wa chini ya miaka 21 Samuel Iling-Junior, 20, ananyatiwa na Tottenham, Aston Villa na Brighton. (Fichajes kwa Kihispania)
Juventus haijakataa kumsajili mlinzi wa zamani wa Ureno Tiago Djalo, 23, kutoka Lille ya Ufaransa mwezi Januari, lakini huenda ukafanya hivyo siku za usoni. (Gazzetta dello Sport kwa Kiitaliano)
West Ham na Fulham wanamtaka mshambuliaji wa Nigeria Akor Adams, 23, ambaye huenda akaondoka Montpellier mwezi Januari kwa ada ya takriban £15-20m. (Football Insider)
Nottingham Forest imekubali dau la zaidi ya euro 5m (£4.3m) kutoka kwa Atletico Mineiro kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Gustavo Scarpa, 29. (Fabrizio Romano)
Brentford, Crystal Palace na Fulham wanamuwania mshambuliaji wa Getafe, 26, Mhispania Borja Mayoral, 26. (Fichajes - kwa Kihispania)
Chelsea wamekubaliana na Darou Salam kumsajili kiungo wao wa kati kutoka Senegal Pape Daouda Diong,17. (90 min)
BBC



