Manchester City wanaendeleza mazungumzo kuhusu kumnunua kiungo wa klabu ya River Plate, 17, Claudio Echeverri, huku Chelsea pia ikimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina. (Fabrizio Romano)
Echeverri ana kipengele cha kuachiliwa cha pauni milioni 21.4 katika mkataba wake huku City wakipanga kumrudisha kwa mkopo River mara moja. (Times - usajili unahitajika)
Barcelona wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Manchester City kuwania saini ya kiungo wa Fluminense Andre, 22, huku Pep Guardiola akimtambua Mbrazil huyo, ambaye pia anahusishwa na Liverpool na Fulham, kama mchezaji anayetarajiwa kusajiliwa kwa siku zijazo. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Klabu za Ligi ya Primia zinatazamiwa kukabiliwa na wimbi jipya la kutaka kuwanunua wachezaji wao wakuu kutoka Ligi kuu ya Saudia huku idadi ya wachezaji wa kigeni inayoruhusiwa katika vikosi vyao kuongezeka kutoka wanane hadi 10. (Daily Telegraph - usajili unahitajika)
Manchester United wameungana na Manchester City na Liverpool katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Joshua Kimmich, 28, kutoka Bayern Munich. (Fichajes - kwa Kihispania)
Arsenal wako tayari kumuuza na mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah, 24, kwa ada ya takriban £40m huku West Ham, Brentford na Crystal Palace wakimuwania. (Football Insider)
AC Milan itasalia na kocha Stefano Pioli kwa wakati huu, licha ya meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte kuonekana kama mbadala wa msimu ujao. (Gazetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester United wamemweka kiungo mkabaji wa Lyon Rayan Cherki, 20, kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa huku mkufunzi Erik ten Hag pia akitaka kusajili mshambuliaji pamoja na Mfaransa huyo. (Football transfer)
Manchester City wanaitaka Barcelona kulipa zaidi ya pauni milioni 26 ili kufanya uhamisho wa mkopo wa mlinzi wa Ureno Joao Cancelo kuwa wa kudumu. (Sport - kwa Kihispania)
Wakala wa mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen amepuuza tetesi kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria ataondoka msimu ujao licha ya kipengele cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 katika kandarasi mpya inayozidi £100m. (Corriere dello Sport kupitia Football Italia)
Manchester United wako tayari kumruhusu winga wa Ivory Coast Amad Diallo kuondoka Old Trafford kwa mkopo mwezi Januari, huku Southampton wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Football Insider)
Paris St-Germain wamekubali ada ya £17.5m (euro 20m) na Sao Paulo kwa ajili ya beki wao wa kati Mbrazil Lucas Beraldo, 20, ambaye pia alikuwa kwenye rada za bosi wa Liverpool Jurgen Klopp. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Kocha wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anakaribia kurejea kwenye uongozi, huku raia wa Norway anayependwa zaidi akipigiwa upatu kuchukua mikoba katika klabu ya Uturuki ya Besiktas. (Mirror)
Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe atafanya mazungumzo na mkurugenzi wa soka Dan Ashworth kuhusu malengo ya uhamisho ya klabu hiyo Januari. (Newcastle Chronicle)
BBC