Kili Stars uso kwa uso na Zanzibar Heroes

Joel JJ By Joel JJ
β€’
25 Dec 2023
Kili Stars uso kwa uso na Zanzibar Heroes

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars', Adel Amrouche ametaja kikosi cha wachezaji 25 watakaoingia kambini leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes'

Mchezo huo utakaopigwa Desemba 27 ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar uliofanyiwa marekebisho makubwa.

Kikosi hicho kinaundwa na makipa Kwesi Kawawa (Karlslunds IF), Beno Kakolanya (Singida Fountain Gate) na Aishi Manula wa Simba huku mabeki wakiwa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job na Nickson Kibabage (Yanga), Israel Mwenda, Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa Simba

Wengine ni Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Adam Kasa (IFK Haninge), Zion Chebe Nditi (Aldershot Town), Mark John (Kingston FC) na Miano Danilo wa Villena CF.

Viungo ni Adolf Bitegeko (Volsungur IF), Yusuph Kagoma (Singida FG), Roberto Yohana (Fofar Athletic), Mzamiru Yassin (Simba), Edwin Balua (Tanzania Prisons), Said Hamis (Jedinstov Ub), Tarryn Allarakhia (Wealdstone) na Sospeter Bajana wa Azam.

Washambuliaji wanaongozwa na Simon Msuva aliyeachana na klabu ya JS Kabylie ya Algeria baada ya kuvunjiwa mkataba mapema Desemba hii, Ladaki Chasambi (Mtibwa Sugar), Kibu Denis (Simba) na Abdul Suleiman 'Sopu' anayekipiga kunako Azam FC.

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
1h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
3h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
4h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
10h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’