Tottenham Hotspur inamfuatilia mshambuliaji wa Bournemouth Muingereza Dominic Solanke, 26, wakati wakitafuta kusajili mshambuliaji msimu wa joto. (Sun)
Newcastle na Juventus ndio wanaongoza kwa sasa katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 28 kutoka Manchester City mwezi ujao. (Football Insider)
Inter Milan wanasonga mbele katika mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Club Bruges wa Canada Tajon Buchanan mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia amezivutia Manchester City na Bournemouth. (Fabrizio Romano)
Meneja wa Manchester United Erik ten Hag amekataa kuthibitisha iwapo mshambuliaji Anthony Martial atauzwa mwezi Januari. (Guardian)
Barcelona wanaweza kukosa kumsajili Estevao Willian wa Palmeiras mwenye umri wa miaka 16 huku Chelsea, Manchester City, Manchester United na Paris St-Germain zikijiandaa kumsajili mlinzi huyo wa Brazil. (Mundo Deportivo)
Aliyekuwa mkurugenzi wa michezo wa Liverpool Julian Ward ameibuka kuwa mgombea wa nafasi kama hiyo katika klabu ya Manchester United. (Telegraph) Real Betis wanapiga hatua katika mpango wa kudumu wa kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United Mhispania Marc Roca, 27, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu hiyo ya Uhispania. (Football Insider)
BBC