Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kikosi kimerejea mazoezini kwa ajili ya michuano ya kombe la Mapinzudi inayoanza kutimua vumbi leo huko Zanzibar
Ahmed amesema Jumapili, Disemba 31 timu itaelekea Zanzibar ikiwa na wachezaji wote ambao hawatakuwa katika majukumu ya timu za Taifa
"Tumeanza maandalizi kwa ajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi. Timu itaondoka Dar Disemba 31 kuelekea Zanzibar tayari kwa michuano hiyo"
"Tunakwenda Zanzibar na wachezaji wote ambao hawatakuwa na majukumu ya timu za Taifa zinazokwenda kushiriki michuano ya Afcon 2023"
"Mashabiki wetu Zanzibar wakae tayari kuipokea timu yao, tunapeleka burudani Zanzibar na lengo letu ni kurejea na kombe Dar," alisema Ahmed
Mchezo wa kwanza wa Simba ni dhidi ya JKU na utapigwa Januari 1 2024 katika uwanja wa Amaan Complex uliozonduliwa rasmi jana baada ya kufanyiwa ukarabati