Transfer - International

Tetesi zaa usajili Ulaya, Alhamisi Disemba 28 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Dec 2023
Tetesi zaa usajili Ulaya, Alhamisi Disemba 28 2023

Newcastle United wana imani kuwa wanaweza kukubaliana kuhusu mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips kutoka Manchester City lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus, Everton na Crystal Palace kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Telegraph)

Familia ya Glazer italazimika kumlipa Sir Jim Ratcliffe hadi $66m (£52m) ikiwa watasitisha mpango wa kampuni yake ya Ineos Group kununua asilimia 25 ya hisa katika Manchester United. (Independent)

Kama sehemu ya mpango huo, Ineos pia inabidi ashauriwe kuhusu uhamisho wowote wa Manchester United katika dirisha la uhamisho la Januari na meneja Erik ten Hag hawezi kufukuzwa kazi bila kuhusika kwa Ratcliffe. (Standard)

Kiungo wa kati wa Ureno Joao Neves, 19, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Manchester United, yuko kwenye mazungumzo kuhusu kandarasi mpya katika klabu ya Benfica ambayo huenda ikaongeza kifungu chake cha kuachiliwa kutoka euro 120m (£104m) hadi euro 150m (£130m). (O Jogo)

United pia inahusishwa na mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres, 25, kutoka kwa wapinzani wa Benfica Sporting Lisbon. (Correio da Manha)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anasema klabu hiyo iko tayari kuimarisha kikosi chake mwezi Januari "kwa sababu tunataka kuwa na nguvu zaidi". (Guardian)

The Gunners wanavutiwa na mlinzi wa kati wa Bayern Munich Matthijs de Ligt lakini huenda kuna uwezekano wa kumnunua Mholanzi huyo wa miaka 24 mwezi Januari. (Athletic)

Liverpool wamewauliza Fulham kuhusu kupatikana kwa mchezaji wa kimataifa wa Marekani Antonee Robinson, 26, huku wakitafuta kusajili mlinzi wa kushoto katika dirisha la uhamisho la Januari. (90min)

Tottenham wamewaambia mlinzi wa Uingereza Eric Dier, 29, kiungo wa kati wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, na mlinda lango Mfaransa Hugo Lloris, 37, kwamba wanaweza kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari. (Football Insider)

Mshambulizi wa kimataifa wa Ufaransa Antoine Griezmann, 32, anasema Atletico Madrid itakuwa klabu yake ya mwisho barani Ulaya na angependa kumalizia soka lake nchini Marekani. (AS )

Roma wanajaribu kuafikiana mpnngo wa kumsajili mlinzi wa zamani wa Juventus Leonardo Bonucci, huku klabu ya Ujerumani Union Berlin ikiwa tayari kumwachia nyota huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 36 kuondoka bure. (Gazzetta dello Sport)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
10h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
17h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
18h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
19h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
21h ago
READ MORE β†’