Jana klabu ya Azam Fc ilitambulisha usajili wa mshambuliaji Franklin Navarro raia wa Colombia
Navarro anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Colombia kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara
Hii ni ishara kuwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara sasa inapasua anga
Kuna kundi kubwa la wachezaji kutoka nje, hata masafa ya mbali huko Amerika
Msimu uliopita Singida BS ilisajili wachezaji kutoka Brazil na Argentina na sasa tunaona Azam Fc wameenda Colombia
Hata hivyo uzoefu unaonyesha wachezaji hao kutoka America wamekuwa na wakati mgumu kuonyesha umahiri wao hapa Tanzania
Lakini inaweza kuwa tofauti kwa Navarro ambaye anatajwa kuwa mshambuliaji mwenye kasi na jicho la kuliona lango