Simba - Local - Transfer

Simba yatamba kusajili kimya-kimya

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 Dec 2023
Simba yatamba kusajili kimya-kimya

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amewatoka hofu wanachama na mashabiki wa timu hiyo juu ya michakato ya usajili katika dirisha dogo lililofunguliwa Disemba 16 likitarajiwa kufungwa Januari 15 2024

Ahmed amesema michakato ya usajili inaendelea na mpaka sasa kuna wachezaji ambao tayari wamesajiliwa kinachosubiriwa ni utambulisho wao tu

"Wanasimba wasidhani tuko kimya, kuna mambo makubwa yanafanyika nyuma ya pazia. Safari huu tunaleta wachezaji ambao wameiva, sio wachezaji wa kusubiri kwani muda huo haupo"

"Tetesi zimekuwa nyingi lakini muhimu Wanasimba wasubiri taarifa rasmi kutoka katika vyanzo vyetu vya habari"

"Wanasema kimya kingi kina mshindo mkubwa, kuna usajili umefanyika huo utakwenda kujaza maji kwenye mabwawa yote ya kuzalisha umeme na kumaliza kabisa tatizo la mgao wa umeme," alitamba Ahmed

Taarifa za ndani ya uongozi wa Simba zimedokeza kuwa takribani wachezaji watano au sita wataongezwa katika dirisha hili dogo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’