Yanga - Local

Yanga kuanza na Jamhuri Mapinduzi Cup leo

Joel JJ By Joel JJ
31 Dec 2023
Yanga kuanza na Jamhuri Mapinduzi Cup leo

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wanatupa karata yao ya kwanza katika michuano ya kombe la Mapinduzi kwa mchezo dhidi ya Jamhuri ambao utapigwa saa 2:15 usiku katika uwanja wa New Amaan Complex

Wananchi walitua Zanzibar jana wakiwa na msafara uliojumuisha wachezaji 22

Kocha Miguel Gamondi aliongoza kikosi jana jioni katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika uwanja wa Amaan

Ukiangalia benchi la ufundi limekamilika, wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa wamesafiri isipo kuwa Yao Kouassi na Khalid Aucho ambao imeelezwa wana ruhusa maalum

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wanataka kutwaa taji la Mapinduzi msimu huu

Aidha Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kuhakikisha wanawahi mapema uwanja wa Amaan kwani kabla ya mchezo kutakuwa na utambulisho wa mchezaji mpya

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
23m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
12h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
20h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
21h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →