Kikosi cha Simba kimewasili Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi iliyoanza kutimua vumbi siku chache zilizopita
Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha anatarajiwa kuondoka na wachezaji wote ambao hawatakuwa na majukumu ya timu za Taifa
Benchikha amesema atatumia michuano hii kuimarisha kikosi chake
Mchezo wa kwanza wa Simba utapigwa kesho Jumatatu dhidi ya JKU
Simba iko kundi B pamoja na JKU, Singida FG na APR. Hili ndio 'kundi la kifo'



