Yanga - Local

Gamondi ajitetea kipigo kombe la Mapinduzi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Jan 2024
Gamondi ajitetea kipigo kombe la Mapinduzi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hawakuwa bora katika mchezo dhidi ya APR na hivyo kupoteza mchezo huo wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa mabao 3-1

Gamondi amesema walicheza vyema dakika 45 za kwanza lakini wakapoteza mwelekeo katika kipindi cha pili na kuwapa nafasi wapinzani wao kufunga mabao mepesi

Kocha huyo raia wa Argentina amesema licha ya kuondoshwa katika michuano hiyo, imemsaidia kubaini wachezaji ambao wana sifa ya kuendelea kuitumikia Yanga

"Tulikuwa bora katika kipindi cha kwanza lakini mwishoni tukafanya makosa ambayo yaliwapa nafasi APR kusawazisha"

"Kipindi cha pili tulipoteana, yawezekana ni uchovu au baadhi ya wachezaji kutokuwa katika daraja la ushindani sawa na wapinzani wetu"

"Timu yetu imewakosa wachezaji 14, wachezaji nane wamekwenda katika majukumu ya timu za Taifa na wengine wamekosekana kutokana na majeruhi na sababu nyingine"

"Lakini michuano hii imetusaidia kuwapa nafasi wachezaji wetu wa timu ya vijana na wengine ambao hawakutumika sana katika timu yetu ya kwanza"

"Pia imenisaidia kufanya tathmini juu ya uwezo wa baadhi ya wachezaji kuona kama wanastahili kuendelea nasi au la," alisema Gamondi

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
44m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’