Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini Jumatatu ijayo kwa ajili ya maandalizi ya mechi zinazofuata Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu na kombe la FA
Baada ya kuondoshwa katika michuano ya kombe la Mapinduzi, nyota wa Yanga walipewa mapumziko ya takribani wiki moja kabla ya kurejea kuendelea na maandalizi
Ratiba ya michuano mbalimbali inatarajiwa kurejea mwishoni mwa mwezi wa pili baada ya kumalizika kwa michuano ya Afcon 2023 inayoanza Ivory Coast kesho Jumamosi
Katika ratiba hiyo, mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya CR Belouizdad itapigwa Februari 23 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo