Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Januari 12 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Jan 2024
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa Januari 12 2024

Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 19, lakini Brighton watadai ada ya zaidi ya £100m ili kumsajili. (Evening Standard)

Manchester United wanatazama maendeleo ya mshambuliaji wa Ajax na Uholanzi Brian Brobbey, 21. (Mirror)

Baadhi ya watu wakuu katika Real Madrid wanaamini kuwa klabu hiyo inafaa kumsajili mshambuliaji wa Napoli Mnigeria Victor Osimhen, 25, badala ya mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe, 25, kutoka Paris St-Germain (Football Transfers)

Everton wanataka pauni milioni 60 kwa kiungo wao wa kati wa kimataifa wa Ubelgiji Amadou Onana, 22, lakini Arsenal italazimika kuuza mchezaji mwingine kwanza ili kuweza kumnunua. (I newspaper)

Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia imefanya mawasiliano na Aston Villa kuhusu kumsajili beki wao wa pembeni wa kimataifa wa Ufaransa Lucas Digne, 30. (L'Equipe, kwa Kifaransa).

Kiungo wa kati wa Brentford na Nigeria Frank Onyeka, 26, anasakwa na Everton, Fulham na vilabu kadhaa nje ya nchi na anatarajiwa kuruhusiwa kuondoka kwa mkopo. (Guardian)

Arsenal inamshabikia mshambuliaji wa Bologna na Uholanzi wa Chini ya miaka 21 Joshua Zirkzee, 22. (Telegraph, usajili unahitajika)

West Ham wanamfuatilia mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico Santiago Gimenez, 22, ambaye thamani yake ni pauni milioni 30 na Feyenoord . (Times, usajili unahitajika)

West Ham na Crystal Palace wana nia ya kumsajili winga Mwingereza Jack Clarke mwenye umri wa miaka 23 kutoka Sunderland, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 20, huku klabu yake ya zamani Tottenham ikitarajiwa kupata 25% ya ada yoyote ya uhamisho.(Football London)

Burnley wanatafuta mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Chelsea wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21, ambaye ameitwa kutoka kwa mkopo Union Berlin .(Athletic, usajili unahitajika)

West Ham hawana nia ya kumsajili tena kiungo mshambuliaji wa Uingereza Jesse Lingard, 31, ambaye anapatikana kwa uhamisho wa bure. (Standard)

Lyon wanajitahidi sana kumsajili winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma huku winga huyo mwenye umri wa miaka 26 akisubiri Everton kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake baada ya uhamisho wake wa mkopo kutoka Villarreal . (Liverpool Echo)

Leicester City wanajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan na Italia Stefano Sensi, 28. (Leicester Mercury)

Skauti wa Manchester City na Manchester United wamekuwa wakimtazama kiungo wa kati wa FC Copenhagen na Uswidi Roony Bardghji mwenye umri wa miaka 18. (Football Insider)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’