Dirisha dogo la usajili linafungwa leo Jumatatu, saa 5:59 usiku ambapo dirisha hilo limekuwa wazi kwa takribani mwezi mmoja
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha hilo kufungwa
Timu zinapaswa kukamilisha usajili ndani ya muda ikiwa ni pamoja na uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wanaotoka nje ya nchi



