Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain wanavutiwa na beki wa Lille ya Ufaransa aliye chini ya umri wa miaka 21, Leny Yoro, 18. (Telefoot kupitia AS - kwa Kihispania) Brighton wamekamilisha usajili wa beki wa pembeni wa Argentina chini ya umri wa miaka 20, 19, Valentin Barco kutoka Boca Juniors kwa takriban Β£8m. (Telegraph - usajili unahitajika)
Mshambulizi wa Manchester United Anthony Martial yuko tayari kukataa ofa ya Saudi Arabia kwani angependelea kusalia Ulaya, huku West Ham, Inter Milan na Fenerbahce wakihusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 28. (Caught Offside)
Arsenal na Chelsea watamtazama beki wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ivory Coast Ousmane Diomande katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa nia ya kutaka huduma zake (Record - Kwa Kireno)
Mustakabali wa Karim Benzema katika klabu ya Al-Ittihad haujulikani baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 36 kukosa mazoezi na hatimaye kutengwa kwenye kambi ya klabu hiyo ya majira ya baridi kali huko Dubai. (Marca)
Tottenham, Arsenal na Fulham wako tayari kumenyana na West Ham katika uhamisho wa majira ya joto wa mshambuliaji wa Feyenoord wa miaka 22 wa Mexico Santiago Gimenez. (Football Insider)
Everton na Nottingham Forest wanatarajia kuambiwa Jumatatu kwamba wamekiuka kanuni za faida na kanuni za usimamizi wa kifedha wa Premier League kwa mzunguko wa miaka mitatu hadi Juni 2023(The Athletic - usajili unahitajika)
Liverpool wako tayari kumuuza mlinda lango wa Jamhuri ya Ireland, 24, Caoimhin Kelleher kwa pauni milioni 20 msimu huu wa joto na wamemtambua mchezaji wa zamani wa Sunderland wa timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, Anthony Patterson, 23, kama atakayechukua nafasi yake.(Mirror)
Napoli wanavutiwa na mlinzi wa Chelsea Mwingereza Trevoh Chalobah, 24. (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano) Sheffield United wanavutiwa na beki wa Bournemouth wa Wales Chris Mepham, 26. (Sun)
Hannibal Mejbri atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika Sevilla wiki hii baada ya mkataba wa mkopo wenye chaguo la kumnunua kuafikiwa na Manchester United kwa kiungo huyo wa miaka 20 wa Tunisia. (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Bournemouth Muingereza Joe Rothwell, 29, anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu huko Southampton kabla ya kukamilisha uhamisho wa mkopo hadi mwisho wa msimu.(Daily Echo)
Southampton pia wanalenga winga kwa mkopo mwezi huu huku mchezaji wa kimataifa wa Manchester United wa Ivory Coast Amad Diallo, 21, na mchezaji wa kimataifa wa Wales wa Bournemouth David Brooks, 26, akiwa kwenye orodha yao fupi. (Givemesport)
BBC