Dirisha dogo la usajili lililofunguliwa Disemba 16 2023, limefungwa rasmi usiku wa kuamkia leo Januari 16 2024 huku klabu za Yanga na Simba zikikamilisha usajili wa nyota wa kigeni dakika za lala salama
Simba ilifunga usajili kwa kumtambulisha mshambuliaji kinara wa mabao ligi kuu ya Zambia Freddy Michael Kouablan kutoka klabu ya Green Eagles
Nyota huyo raia wa Ivory Coast ana umri wa miaka 25 akiwa mshambuliaji wa pili kusajiliwa na Simba jana baada ya Pa Omar Jobe

Yanga nayo ikajibu mapigo ya watani zao kwa kumtambulisha mshambuliaji Joseph Guede Gnadou raia wa Ivory Coast
Guede ametua Yanga akiwa mchezaji huru baada ya kumalizana na klabu ya Tuzlaspor ya Uturuki
Kabla ya kutimkia Uturuki, Guede aliitumikia FAR Rabat akiwa sehemu ya kikosi kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco msimu uliopita
Aidha Simba imeachana na nyota watatu wa kigeni Jean Baleke, Moses Phiri na Aubin Kramo nafasi zao zikichukuliwa na Jobe, Kouablan na Babacar Sarr
Yanga imeachana na Jesus Moloko na Hafiz Konkoni nafasi zao zikichukuliwa na Augustine Okrah na Guede