Mapema leo, Ihefu Fc ilimtambulisha aliyekuwa CEO wa Singida Fountain Gate, Olabine Sikwane kuwa Mtendaji Mkuu
Kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma na timu hiyo inasema kuwa imemteua Olabine Sikwane kuwa Mtendaji Mkuu na Fred Chalamila kuwa Ofisa Mtendaji Msaidizi
Aidha timu hiyo imemteua Ramadhan Swanzurimo kuwa kuwa Mkurugenzi wa ufundi (Technical Director) ambaye pia alikuwa na cheo hicho Singida FG
Mthias Lule anakuwa Kocha Msaidizi na Themi Felix kuwa Kocha Msaidizi na Meneja wa timu
Zipo taarifa kuwa baadhi ya nyota wa kigeni wa Singida FG wataibukia Ihefu Fc pia
Ihefu Fc imeweka kambi Jijini Arusha ikiwa na kocha Meky Maxime kwaajili ya maandalizi ya Ligi Kuu inayotarajiwa kurejea baada ya mashindano ya AFCON kumalizika
ADVERTISE HERE