Tanzania imepoteza mchezo wa kwanza michuano ya Afcon 2023 ikichapwa mabao 3-0 dhidi ya Morocco
Ghanem Saiss, El-Eddine Ounahi na Youssef En-nesyri walifunga mabao ya Morocco
Ulikuwa mchezo ambao Stars ilicheza kwa kujihami zaidi lakini ilikwenda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0
Kadi ya pili ya njano ilipelekea Novatus Dismas kutolewa nje kwa kadi nyekundu
Haikuwa tena rahisi kwa Stars kwenda na kasi ya Morocco baada ya kuwa pungufu, pengine mambo yangekuwa mabaya zaidi kwa Stars siku ya leo
Stars sasa imebakisha alama sita za kupigania dhidi ya Zambia na DR Congo