Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa, Januari 19 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jan 2024
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa, Januari 19 2024

Manchester United wanafikiria kurekebisha safu yao ya ulinzi katika msimu wa joto jambo ambalo linaweza kumaanisha beki wa kati wa Uingereza Harry Maguire, 30, na mlinzi wa Uswidi Victor Lindelof, 29, kuondoka ikiwa ofa muhimu zitatolewa kwa ajili yao. (ESPN)

Fulham wamewasilisha ombi la pauni milioni 30 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 5 kwa ajili ya kiungo wa Fluminense Andre, 22, huku The Cottagers wakiwa tayari wamekubaliana na mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Ben Jacobs)

Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim anasema Chelsea italazimika kuanzisha kipengele cha kutolewa cha euro 100m (£85.6m) kwa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres ikiwa wanataka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 25 (Goal)

West Ham ni moja ya klabu zinazovutiwa na kiungo wa kati wa Manchester City Kalvin Phillips na The Hammers wako katika nafasi nzuri ya kushinda katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 28(Standard)

Manchester City wana nia kubwa ya kumrejesha beki wa kulia wa Tottenham na Uhispania Pedro Porro, 24, na kiungo wa kati wa Aston Villa na Brazil Douglas Luiz, 25, katika klabu hiyo kwa mikataba ambayo inaweza kuwagharimu £200m. (Football Insider)

Klabu ya Ufaransa Lyon inajaribu kumsajili winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma, 26, ambaye alijiunga na Everton kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Villarreal msimu uliopita wa joto. (Liverpool Echo)

Mshambulizi Mfaransa Karim Benzema yuko tayari kuihama klabu ya Saudi Pro League ya Al-Ittihad lakini, wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anaamini kuwa huenda akahamia Uingereza, mshahara wake unaweza kuwa kikwazo kwa uwezekano wowote wa kuhamia Arsenal au Chelsea. (Standard)

Aston Villa wameanzisha ombi la kumnunua winga wa Middlesbrough Morgan Rogers, 21, huku meneja Unai Emery akimtaka mchezaji huyo ambaye ameiwakilisha Uingereza katika ngazi ya vijana (Independent)

Mchezaji wa Tottenham James Maddison, 27, analenga kurejea kutoka kwa jeraha la goti kwa timu yake katika mchezo wa raundi ya nne ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City mnamo Ijumaa, 26 Januari. (Telegraph - usajili unahitajika)

Leeds United wanafanyia kazi mkataba wa kudumu kumsaini mlinzi aliyeko kwa mkopo wa Tottenham na Wales Joe Rodon, 26, ambaye thamani yake ni zaidi ya £15m. (Football Insider)

Mshambuliaji wa Italia Moise Kean, 23, anakaribia kuhama kwa mkopo kutoka Juventus kwenda Atletico Madrid. (Sky Sports Italia)

Kiungo wa kati wa Everton Amadou Onana amekuwa akihusishwa na Arsenal lakini mkufunzi wa Toffees Sean Dyche amepuuza uvumi unaomhusisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22 kuondoka. (90 Min)

Beki wa Uhispania Javier Manquillo, 29, anakaribia kuondoka Newcastle United na kujiunga na klabu ya La Liga Celta Vigo. (Athletic -Usajili unahitajika)

BBC

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’