Bado Tanzania haijafanikiwa kupata ushindi katika michuano ya Afcon leo ikilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia iliyocheza pungufu kwa muda mrefu
Ilibaki kidogo Stars kuondoka na alama tatu kama sio bao la Patson Daka aliyeisawazishia Zambia katika dakika ya 86 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Clatous Chama
Ilikuwa Tanzania iliyotangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 11 Simon Msuva akimalizia pasi kutoka kwa nahodha Mbwana Samatta
Pengine Stars watajilaumu kwa kukosa ushindi katika mchezo huo, walitawala hasa ikingatiwa Zambia walikuwa pungufu kwa muda mwingi wa mchezo
Stars sasa inahitaji kushinda mchezo wa mwisho dhidi ya DR Congo ili kuwa na nafasi ya kutinga hatua inayofuata