Safari ya Tanzania katika michuano ya Afcon 2023 imehitimishwa na suluhu ya bila kufungana dhidi ya DR Congo
Ulikuwa mchezo ambao Tanzania ilihitaji ushindi ili kukata tiketi ya hatua ya mtoano hata hivyo safu ya ushambuliaji imekuwa changamoto kubwa kwa Tanzania katika michuano hiyo
DR Congo na Morocco zimetinga hatua ya mtoano baada ya kushika nafasi ya pili na ya kwanza kundi F
Morocco iliichapa Zambia bao 1-0 katika mchezo mwingine uliohitimishwa leo
Hadi wakati mwingine tena kwa Stars na Zambia katika michuano ya Afcon 2023