Ni rasmi sasa Rais wa Yanga Injinia Hersi Said leo amezindua ofisi za klabu ya Yanga zilizo ndani ya jengo la klabu hiyo lililoko mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Hamis Mwinjuma alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Kuanzia leo shughuli zote za klabu zitafanyika Jangwani ambapo Watendaji wote watakuwa na ofisi katika jengo hilo
Hersi amewakaribisha Wanachama na Mashabiki wa Yanga kupata huduma mbalimbali katika ofisi zao za kisasa kabisa






