Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 12, 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Feb 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 12, 2024

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 25, bado hajakubali masharti ya kujiunga na Real Madrid mkataba wake utakapomalizika huku klabu hiyo ya La Liga ikihangaika kufanya mazungumzo na mamake mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, na wakala, Fayza Lamari. (Marca)

Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelotti amedokeza kuwa timu hiyo haimhitaji Mbappe kwani tayari wana "wachezaji sita bora duniani". (Goal)

Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia winga wa Athletic Bilbao Nico Williams, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 akionekana kuwa bora kwa Ligi ya Premia. (Fabrizio Romano, via CaughtOffside)

Kinda wa AC Milan Francesco Camarda atatia saini mkataba wake wa kwanza wa kitaalamu na Rossoneri wakati chipukizi huyo wa Kiitaliano atakapofikisha umri wa miaka 16 mwezi ujao licha ya Manchester City na Borussia Dortmund kumtaka. (Calciomercato, via Football Italia)

Newcastle wanafikiria kumsajili beki wa Bournemouth Lloyd Kelly, 25, msimu huu wa joto. (Mail)

Barcelona hawana nia ya kumruhusu mshambuliaji wa Uhispania Ferran Torres, 23, kuhama klabu hiyo msimu wa joto. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Jose Mourinho, 61, yuko tayari kuchukua nafasi ya meneja wa Bayern Munich ikiwa klabu hiyo itaamua kumfukuza Thomas Tuchel, 50. (Bild - kwa Kijerumani)

Liverpool wako tayari kumpa mlinzi wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 25, mkataba mpya wa muda mrefu. (Football Insider)

Liverpool wanamfuatilia mlinzi wa Fulham Tosin Adarabioyo, 26, kwa ajili ya uhamisho unaowezekana msimu huu wa joto. (Mail)

Sheffield Wednesday wanapania kuwasilisha ofa ya kumnunua mshambuliaji wa Orlando City na Marekani Duncan McGuire, 23, ikiwa klabu hiyo haitashushwa daraja msimu huu. (Sun)

Kiungo wa kati wa Uturuki na Lille Yusuf Yazici anawaniwa na klabu kadhaa za Ulaya, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 akielekea kuiondoka klabu hiyo ya Ufaransa mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)

Rais wa La Liga Javier Tebas, 61, anasema mshambuliaji wa Argentina na Inter Miami Lionel Messi, 36, alikuwa "karibu" kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Barcelona msimu uliopita. (Mirror)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’