Kikosi cha Yanga leo kinaelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa Jumamosi, Februari 17 katika uwanja wa Jamhuri
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema timu inakwenda Morogoro ikiwa na lengo moja tu, kwenda kusaka alama tatu dhidi ya KMC
"Tumepata muda wa kufanya maandalizi ya mchezo huu. Wachezaji wote tuliowasajili msimu huu wameshiriki maandalizi, kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu hakuna mchezaji anayekosekana kutokana na majeruhi au sababu nyingine"
"Tunaamini kwa maandalizi tuliyofanya, tunakwenda Morogoro kuchukua alama tatu dhidi ya KMC," alisema Walter ambaye amewahi kuwa Mtendaji wa KMC
Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa mlindda lango Metacha Mnata ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons
Hata hivyo habari njema kwa Wananchi ni urejeo wa Djigui Diarra ambaye alirejea nchini mwanzoni mwa wiki hii baada ya kumaliza majukumu ya timu ya Taifa