Wekundu wa Msimbazi Simba Sc leo wanaendelea na kampeni ya kusaka ubingwa wa ligi kuu 2023/24 wakiwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Meja Jen. Isamuhyo huko Mbweni
Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kucheza katika uwanja huo ulio ndani ya kambi ya Jeshi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amewataka mashabiki wa Simba kuchangamkia tiketi 4000 ambazo zitauzwa kwa mashabiki
Uwanja wa Meja Jen. Isamuhyo una uwezo wa kuchukua mashabiki 4000 waliosimama na viti 200 kwa ajili ya VIP
Huu ni mchezo wa kiporo wa kukamilisha mechi 15 za duru ya kwanza