Yanga - Local

Meneja amshukia Mayele

Joel JJ By Joel JJ
β€’
15 Feb 2024
Meneja amshukia Mayele

Nestor Mutuale ndiye Meneja wa mshambuliaji Fiston Mayele, katika mahojiano na Wasafi Media, ameeleza masikitiko yake kutokana na kauli zilizotolewa na Mayele katika mitandao ya kijamii

Mutuale amesema hata kama Mayele atakuwa amekasirishwa na baadhi ya mashabiki au kiongozi fulani, hakuwa sahihi kuisema vibaya timu ya Yanga ambayo ina mchango mkubwa kwenye maendeleo yake.

"Nimeona mitandao ya Tanzania inasema hayo mambo kwamba Mayele anaisema vibaya Yanga, sijaongea naye tangu wamerudi hapa nchini kutoka Ivory Coast, lakini kama kweli hayo maneno ameyasema yeye atakuwa ameikosea heshima Yanga"

"Wachezaji hawatakiwi kuwajibu mashabiki hasa mitandaoni, shabiki anaweza kusema lolote, mchezaji unatakiwa kuvumilia na kuendelea kufanya kazi yako, kule uwanjani ndio unatakiwa kuwajibu mashabiki"

"Yanga haiwezi kufanya kitu kibaya kwa Mayele, kama kuna shabiki amemtolea lugha chafu Mayele atakuwa amekosea lakini Mayele kuisema vibaya Yanga ni makosa makubwa amefanya"

"Unajua Yanga imefanya makubwa kwa Mayele, ule upendo walimpa ni wa kiwango kikubwa sana, wapo watoto, wakubwa, viongozi na maelfu ya mashabiki wamekuwa wakimpenda Mayele kutokana na kazi yake, unapotaka kusema kitu kibaya kuhusu mtu mmoja unatakiwa kuwaangalia hawa wengi watajisikiaje"

Aidha, Mutuale amewataka mashabiki wa Yanga kumsamehe Mayele kwani atakuwa amejifunza kuwa amekosea kwani bado ni mtoto wao ambaye siku moja wanaweza kukutana naye tena.

"Mimi nitamtafuta Mayele nitaongea naye, nimeongea na viongozi wa Yanga wamesikitika, lakini nimewaambia wamsamehe Mayele na mashabiki nao wamsamehe ni mtoto wao amewakosea hawawezi kusema sio ndugu yao tena, maisha yanaweza siku moja tena yakamfanya arudi tena nyumbani kwao Yanga," alisema Nestor

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
32m ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
10h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
14h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
18h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
19h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
20h ago
READ MORE β†’