Baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa mkoani Morogoro, Wananchi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Ni Jumamosi ya Februari 24, Yanga itakuwa mwenyeji wa CR Belouizdad katika mchezo wa raundi ya tano kundi D utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku
Hii ni kama fainali kwa Yanga kwani Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Yanga itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza ulioipigwa Algeria
Hivyo hii ni mechi ya kisasi, deni inapaswa lilipwe mbele ya mashabiki 60,000 ambao wanatarajiwa kujitokeza kuishangilia Yanga
Aidha ushindi wa zaidi ya mabao 3 unaweza kutosha kuipeleka Yanga robo fainali hasa kama itatokea Medeama watakosa ushindi dhidi ya Al Ahly katika mchezo utakaopigwa Februari 23 huko Ghana
Katika msimamo wa kundi D, Al Ahly wako kileleni wakiwa na alama sita, Belouizdad iko nafasi ya pili ikiwa na alama tano sawa na Yanga timu hizo zikitofautiana mabao
Medeama wako nafasi ya nne wakiwa na alama nne. KIla timu kundi D ina nafasi ya kwenda robo fainali