Kikosi cha Simba jana kilifanya mazoezi ya kwanza nchini Ivory Coast kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Asec Mimosas utakaopigwa kesho Ijumaa
Ari na morali ya vijana wa kocha Abdelhak Benchikha iko juu mkakati ukiwa kuzisaka alama tatu dhidi ya Asec na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali
Leo Simba itafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Felix Houphouet Boigny ambao utatumika Ijumaa
Simba itaanza mazoezi yake saa 4 usiku (saa 1 Ivory Coast) sawa na muda ambao mchezo huo utachezwa













