Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 22 2024

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd February 2024


Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Februari 22 2024

Chelsea inaongoza Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen mwenye umri wa miaka 25 msimu unaokuja. (TeamTalks)

West Ham wanatazamia kumnunua mshambuliaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 26 Dominic Solanke. (Telegraph – Subscription Required)

Meneja wa Bayern Munich Thomas Tuchel atapa kipaumbele kurejea Uingereza atakapoondoka katika klabu hiyo ya Ujerumani mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph – Subscription Required)

Jurgen Klopp hatachukua nafasi ya Tuchel katika klabu ya Bayern Munich atakapoondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa wakala wa meneja wa Liverpool. (Sky Sports Germany)

Mshambulizi wa AC Milan na Ufaransa Olivier Giroud, 37, anaweza kuondoka katika klabu hiyo na kwenda MLS mwishoni mwa msimu huu. (Corriere dello Sport – Via Itali)

Chelsea itasikiliza ofa kwa mlinda mlango wa Uhispania Robert Sanchez msimu huu wa joto na The Blues wanaweza kutafuta kuchukua nafasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Football Insider)

Lakini The Blues hawatoi ofa kwa mlinzi wa Uingereza Levi Colwill, 20, ambaye analengwa na Paris St-Germain na Liverpool. (Standard)

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto. (Bild – In Deutsch)

Al-Ittihad itamlenga mshambuliaji wa Tottenham mwenye umri wa miaka 31 Son Heung-min na mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 31 kutoka Misri Mohamed Salah katika dirisha la usajili la kiangazi. (Football Transfers)

Manchester United na Arsenal wanamtaka mshambuliaji wa Bayern Munich Mfaransa mwenye umri wa miaka 18, Mathys Tel. (Bild – In Germany)

Kiungo wa kati wa Everton James Garner analengwa na Tottenham na Newcastle, huku Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 22 akivutia pande nyingi za Ligi ya Premia. (Football Insider)

Liverpool wanatumai kuwa wanapewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Luis Guilherme mwenye umri wa miaka 18 kutoka Palmeiras msimu huu wa joto. (Football Insider)

Chelsea na Arsenal wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Aberdeen Lewis Carrol, 15, mwishoni mwa msimu huu. (Athletic)

BBC


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.