Yanga yasaka robo fainali CAF CL dhidi ya CR Belouizdad

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th February 2024


Yanga yasaka robo fainali CAF CL dhidi ya CR Belouizdad

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga leo wanatupa karata muhimu katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad

Mechi hiyo ya raundi ya tano kundi D, itapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1 usiku

Dakika 90 za mchezo huo zitaamua hatma ya mkakati wa Yanga kuwania tiketi ya kufuzu robo fainali ya michuano hiyo

Baada ya Medeama kupoteza mchezo dhidi ya Al Ahly jana, ushindi mnono kwa Yanga leo unaweza kuwavusha hatua ya robo fainali moja kwa moja kabla ya mechi ya mwisho dhidi ya Al Ahly

Wananchi wanahitaji ushindi wa angalau mabao 4-0 ili kutinga robo fainali. Ushindi mwingine wowote bado utakuwa na faida kwa Yanga lakini ili kujihakikishia kutinga robo fainali, Yanga itahitaji angalau alama moja katika mchezo wa mwisho

Hivyo ni wazi Yanga leo itahitaji kupambana ili kumaliza kazi hapahapa nyumbani kwani mechi ya mwisho dhidi ya Al Ahly ni ugenini

Leo matarajio ni kuona 'full house' kwa Mkapa na muhimu ni mashabiki kuhakikisha wanashangilia kwa dakika zote 90 za mchezo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.