Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 26 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Feb 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu Februari 26 2024

Kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher anataka kusalia Stamford Bridge. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 amebakiza miezi 18 katika mkataba wake na amekuwa akihusishwa na kuhamia Tottenham. (Sky Sports)

Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa Brighton na Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 19, huku wakipania kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu wa joto. (Football Insider)

Mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Edu anasema klabu hiyo "tayari ina malengo yetu" alipoulizwa kuhusu The Gunners kusajili mshambuliaji mpya. (TNT Sports, via Standard)

Mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen anaweza kuwa chaguo kwa Arsenal lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea na Paris St-Germain kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 25. (GiveMeSport)

Kiungo wa kati wa Uingereza Jack Harrison, 27, anataka kubadilisha uhamisho wake wa mkopo kutoka Leeds United hadi Everton kuwa mkataba wa kudumu msimu huu wa joto hata kama timu hiyo ya Elland Road itapandishwa daraja na kurejea Ligi Kuu ya Uingereza. (Football Insider)

Mwekezaji mpya wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe anataka mfumo mpya wa malipo utambulishwe katika klabu hiyo, huku mishahara ya wachezaji ikitegemea zaidi mafanikio. (Mirror)

Manchester United wanalenga kusajili mshambuliaji, mabeki wawili wakati wa marekebisho ya kikosi cha klabu hiyo ya Old Trafford majira ya kiangazi. (Telegraph - usajili unahitajika)

Juventus wameweka bei ya pauni milioni 51 kumnunua Kenan Yildiz anayewindwa na Arsenal. Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 18 amecheza mechi 15 pekee akiwa na Juventus tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Bayern Munich mwaka wa 2022. (Sun)

Mshambuliaji wa Brazil Endrick anatazamiwa kujiunga na Real Madrid atakapofikisha umri wa miaka 18 mwezi Julai, lakini Palmeiras wanajaribu kumbakisha hadi Desemba. (ESPN)

BBC

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
2m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
31m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’