Yanga kuifuata Al Ahly leo

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Feb 2024
Yanga kuifuata Al Ahly leo

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kikosi cha Yanga kitaondoka nchini leo kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly. Mchezo huo utapigwa Ijumaa, March 1, saa 1 usiku kwa saa za Tanzania

Kamwe ametangaza ratiba nzima ya safari ya Yanga ambayo itaanza majira ya saa 11 na dakika 55 jioni ya leo

"Tutaondoka hapa Tanzania saa 11:55 jioni kwa Shirika la Ndege la Ethiopia. Tutapumzika Ethiopia kwa masaa mawili kabla ya kupanda ndege ya kuelekea Cairo ambapo tutawasili Cairo majira ya saa 7 usiku"

"Timu itafikia Hotel ya Royal Kempisky yenye hadhi ya nyota tano. Tunaondoka na msafara wa watu 60 utakaojumuisha wachezaji 24, benchi la ufundi 13 na viongozi na waandamizi wengine 23"

"Hatuendi Cairo kushangaa Pyramids bali tunakwenda kutafuta ushindi ili tumalize vinara wa kundi. Tunataka tuwe wa kwanza katika msimamo ili tupate nafasi ya kucheza dhidi ya timu itakayomaliza nafasi ya pili katika makundi mengine"

"Lakini pia tunataka ushindi ili tupate nafasi ya kuanzia ugenini katika mchezo wetu wa robo fainali. Kushinda dhidi ya Al Ahly kwao itakuwa rekodi kupata ushindi katika ardhi ya Misri," alisema Kamwe

Kamwe ametangaza kuhakikisha Wananchi wanapata fursa ya kushuhudia mchezo huo pamoja hivyo wameandaa utaratibu pale Makao Makuu ya klabu, Jangwani

"Siku ya Ijumaa, Makao Makuu ya klabu, Jangwani tutafunga 'Big Screen' kwa ajili ya Wanachama, Mashabiki na wapenzi wa Yanga ili kuja kufurahia hili jambo pamoja"

Katika hatua nyingine Kamwe amewapongeza wanafamilia wa Yanga kwa kufanikisha Pacome Day

"Nawapongeza benchi la ufundi na wachezaji kwa kufanikisha malengo yetu ya kufuzu robo fainali. Benchi la ufundi limefanya kazi kubwa ya kuiandaa timu yetu na matokeo yake tumefuzu"

"Haikuwa rahisi kufunga mabao 4 dhidi ya CR Belouizdad ambayo imecheza dakika 180 dhidi ya Al Ahly pasipo kuruhusu bao"

"Mchezo wao wa mwisho dhidi ya Al Ahly uliopigwa Algeria Al Ahly hawakupiga hata shoot on-target. Ushindi huu umeonyesha ni kwa kiasi gani Yanga imeandaliwa kushindana"

"Lakini pia nawapongeza Wanachama na Mashabiki kwa kuifanya Pacome Day kufana. Hili ndio tukio kubwa zaidi la michezo lililofanyika katika mechi za CAF mwishoni mwa wiki. Rais wa nchi Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema Yanga imefurahisha nchi, hivyo ni wajibu wetu kuendelea kufurahisha nchi" alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

More Stories

Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
7m ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
52m ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
1h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
5h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
7h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
8h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
10h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
10h ago
READ MORE β†’