Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amesema ni lazima wafanye maandalizi mazuri ili kuweza kupata ushindi katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy
Benchikha amesema Jwaneng wamedhihirisha ni timu isiyotabirika hivyo hawapswi 'kubweteka' na kudhani watakuwa na mechi nyepesi siku ya Jumamosi
"Galaxy sio timu rahisi ni kama jeshi lisilotabirika, hakuna aliyedhani kama ingeifunga Wydad Casablanca nchini Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi, hata hapa Simba rekodi zinaonyesha wamewahi kushtua kwa kushinda hapa"
"Nadhani mashabiki na hata wachezaji wanalijua hili na tayari nimeshakaa kikao na wachezaji na kuwakumbusha. Kwenye soka mambo ya kushtua huwa yanatokea, sitaki historia hii ijirudie hapa chini yangu"
"Nimezungumza nao tukiwa kule ugenini juzi nadhani kila mtu ataelewa tulizungumza nini. Tunatakiwa kujipanga na vita nzito ya mchezo huu, nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kuwapa hamasa wachezaji wao wakiwa vitani ndio kitu pekee tunahitaji kutoka kwao"
"Ili kushinda tunahitaji kufunga mabao ya kutosha lakini pia kujilinda vizuri lakini kule mbele bado hatujawa imara zaidi tutawaongezea wachezaji mbinu za kutengeneza nafasi na kuzitumia kwenye hizi siku tutakazokuwa kambini, " alisema