Kocha Mkuu wa Simba Abdelhakh Benchikha amesema mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy utakuwa kama fainali kwao na wamejipanga kushinda
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari, Benchikha alisema ukiondoa Asec Mimosas, timu nyingine tatu zina nafasi ya kufuzu
"Tunakwenda kucheza mechi muhimu dhidi ya Jwaneng Galaxy. Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu kila timu inawania matokeo mazuri iweze kutinga robo fainali"
"Katika kundi letu ni Asec Mimosas tu ambao wamejihakikishia kufuzu. Wydad wana nafasi ya kufuzu lakini lazima washinde dhidi ya Asec na kusubiri matokeo yetu. Jwaneng wana nafasi ya kufuzu lakini ni lazima washinde na kusubiri matokeo ya mchezo wa Wydad"
"Lakini sisi (Simba) kama tutashinda basi moja kwa moja tutafuzu pasipo kusubiri matokeo ya timu nyingine"
"Nina imani kubwa na wachezaji wangu, pamoja na sapoti ya mashabiki wetu ni lazima tushinde mchezo huu ili tufuzu robo fainali tuwape furaha mashabiki wetu," alisema Benchikha
Mchezo dhidi ya Jwaneng utapigwa Jumamosi, saa 1 usiku



