Transfer - International

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi March 7 2024

Joel JJ By Joel JJ
7 Mar 2024
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi March 7 2024

Barcelona bado wanavutiwa na kocha wa Arsenal Mikel Arteta kuchukua nafasi ya Xavi, ambaye anaondoka mwishoni mwa msimu huu, lakini klabu hiyo ya Uhispania inajua itakuwa vigumu kumteua. (Relevo)

Kocha wa England Gareth Southgate na mkufunzi wa Brentford Thomas Frank ni miongoni mwa chaguzi zinazozingatiwa na Manchester United ikiwa watachagua kuchukua nafasi ya Erik ten Hag mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)

Liverpool, Arsenal na Manchester City wanapigana vikumbo kumsajili kiungo wa Bayern Munich Joshua Kimmich. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 anatazamia kuondoka Bavaria msimu huu wa joto. (Express)

Klabu yoyote inayotaka kumwajiri kocha mkuu wa Brighton Roberto de Zerbi msimu huu wa joto italazimika kuwalipa Seagulls £12.8m. Barcelona, Liverpool na Manchester United wamehusishwa na Muitaliano huyo. (Mirror)

Bayern Munich wako mbele ya Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumteua Xabi Alonso kama kocha wao mwingine ikiwa Muhispania huyo ataamua kuondoka Bayer Leverkusen msimu wa joto. (Telegraph)

Liverpool wana nia ya kumteua Richard Hughes kama mkurugenzi wa michezo baada ya yeye mwenyewe 44, kuthibitisha kuwa ataacha nafasi yake kama mkurugenzi wa kiufundi wa Bournemouth mwishoni mwa msimu huu. (Times)

Liverpool, Borussia Dortmund na Paris St-Germain wanamtaka kiungo wa kati wa Argentina Alan Varela, 22, lakini watalazimika kulipa Porto kifungu chake cha pauni milioni 60. (Mercato)

Kiungo wa kati wa Brazil Joelinton anataka kusalia katika Ligi ya Premia ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 hatakubali mkataba mpya zaidi ya 2025 na Newcastle United. (Football Insider)

Chelsea wanataka kumsajili winga wa Athletic Bilbao Nico Williams. Mshambuliaji huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 21 ana kipengele cha kutolewa ambacho kinaweza kumaanisha kuwa anapatikana kwa pauni milioni 43 msimu huu wa joto. (Telegraph)

Williams pia yuko kwenye rada za Arsenal huku winga wa Wolves Mreno Pedro Neto mwenye umri wa miaka 23 na mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 27, wakizingatiwa pia. (Evening Standard)

West Ham wamepewa nafasi ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund Mjerumani Marco Reus, 34, mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. (Football Insider) Kiungo wa kati wa Ajax Jordan Henderson, 33, hajutii kuondoka Liverpool, akisema ulikuwa "uamuzi bora" kwa pande zote. (Guardian)

BBC

More Stories

SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1m ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
12h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
12h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
16h ago
READ MORE →
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
19h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
21h ago
READ MORE →