Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amerejea Algeria kuhudhuria mafunzo maalum ambapo atakuwa nchini humo kwa siku tano
Benchikha aliondoka mkoani Morogoro jana baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na ameondoka Dar es salaam kuelekea Algeria
Klabu ya Simba imethibitisha kuondoka kwa Benchikha akitarajiwa kurejea nchini baada ya kumaliza mafunzo hayo
Benchikha atazikosa mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Coastal Union na Singida Fountain Gate zitakazochezwa Machi 9 na 12, 2024
Katika kipindi hicho Benchikha amemuachia mikoba msaidizi wake, Farid Zemiti akishirikiana na benchi lake kukiongoza kikosi