Yanga - Mamelodi - Local

Gamondi anaamini Mamelodi wanafungika

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Mar 2024
Gamondi anaamini Mamelodi wanafungika

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kikosi chake kina nafasi ya kupata ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns na kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Ukifuatilia mijadala mbalimbali hasa katika mitandao ya kijamii, utaona wengi wanaipa Yanga nafasi ndogo ya kuvuka mbele ya Mamelodi hata hivyo Gamondi anaamini hakuna jambo lisilowezekana kwa sababu ni wachezaji 11 kwa kila timu watakuwa uwanjani

Yanga itaikaribisha Mamelodi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa March 30 na baada ya hapo timu hizo zitarudiana Aprili 5, mwaka huu, nchini Afrika Kusini na mshindi wa jumla atatinga nusu fainali

Gamondi aliyewahi kuinoa Mamelodi, amesema hana wasiwasi wowote kukabiliana na waajiri wake hao wa zamani akiamini wachezaji wake watakuwa tayari kukabiliana nao

 "Muhimu kwetu ni kujipanga na kuweka juhudi, hatuna sababu ya kuhofia mchezo huu kwa sababu kila timu itakuwa na wachezaji 11 na dakika 90 zitachezwa nyumbani na ugenini"

"Jambo pekee ambalo linaweza kutusumbua kidogo ni uzoefu wa baadhi ya wachezaji katika michuano hii lakini pia naamini tunao wachezaji ambao wamecheza ngazi kama hii ya mashindano ambao uwepo wao utasaidia kuwajenga wale wengine, " alisema 

Kwa miaka ya karibuni Mamelodi Sundowns imekuwa ikipata wapinzani kutoka Afrika Kaskazini katika hatua ya mtoano, mara ya mwisho kuwa na upinzani Kusini mwa Jangwa la Sahara ilikuwa msimu wa 2021/22 walipotupwa nje na Petro Atletico

Pengine hii inaweza kuwa nafasi pia kwa Yanga kuwaduwaza wababe hao wa soka la Afrika Kusini ambao wanasaka taji la pili la Ligi ya Mabingwa wakishinda taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2016

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’