Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, March 21 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Mar 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, March 21 2024

Tottenham wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na England, Conor Gallagher, 24, ambaye mkataba wake unamalizika 2025. (Teamtalk)

Liverpool, Tottenham na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vinavyomuhitaji mlinzi wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, hata hivyo Fullham wanataka kumpa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City mkataba mpya. (Standard)

Tottenham pia wanavutiwa na winga wa Barcelona na Brazil Raphinha, 27, ambaye mustakabali wake katika klabu hiyo ya La Liga hauko wazi. (Sport)

Liverpool, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyohitaji kumnunua beki wa Nottingham Forest raia wa Brazil Murillo, 21. (Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester United, Kobbie Mainoo, 18, anakaribia kusaini mkataba mpya na Red Devils. (HITC)

Beki wa Brazil Thiago Silva, 39, anawasiliana na klabu yake ya zamani ya Fluminense huku akitarajiwa kurejea nyumbani, mkataba wake Chelsea utakapokamilika mwishoni mwa msimu kiangazi. (Sun)

Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe, meneja wa zamani wa Chelsea Graham Potter na Gary O'Neil wa Wolves wote wanaweza kuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kibarua cha kuinoa Engaland iwapo Gareth Southgate ataondoka kwenda Manchester United. (Mirror)

Bayern Munich wanaweza kumgeukia Jose Mourinho, ambaye hana kazi baada ya kutimuliwa Roma, kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka ikiwa hawataweza kumpata Xabi Alonso anayelengwa. (Mirror)

Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte pia anasakwa na Bayern Munich. (Le Repubblica)

Leeds United iko tayari kumpa kiungo Archie Gray, 18, mkataba ulioboreshwa katika msimu wa joto huku kukiwa na vilabu sita vikubwa vya Ligi Kuu ya Uingereza League vinavyotaka kumnunua. (Football Insider)

Winga wa Benfica na Argentina, Angel di Maria, 36, anafikiria kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Rosario Central . (ESPN)

Mlinzi wa Manchester United, Msweden, Victor Lindelof, 29, anasema hana hamu ya kucheza Saudi Arabia bado, licha ya kuhusishwa na kuhamia ligi ya nchi hiyo msimu wa joto. (Fotbollskanalen)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
45m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
8h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’