Tutamfunga Mamelodi kwa Mkapa - Kamwe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Mar 2024
Tutamfunga Mamelodi kwa Mkapa - Kamwe

Kuelekea mchezo wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema hakuna shaka ya aina yoyote wanaenda kushinda mchezo wao dhidi ya Mamelodi Sundowns kwani wana wachezaji bora kuliko timu hiyo.

Akizungumza kwa majigambo katika ofisi za Makao Makuu ya Yanga, Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam, Kamwe amesema wanaelekea katika mchezo huo utakaopigwa Machi 30, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa huku wakitambua fika wachambuzi wengi na waandishi hawaipi nafasi Yanga kushinda mchezo huo.

"Nina uhakika wachezaji sita mpaka saba wanaweza kuanza kwenye kikosi cha Mamelodi. Tunaichukulia poa Young Africans SC kwa sababu tu inatokea Tanzania. Lakini hii Klabu ingekuwa ipo DR Congo ingesifiwa sana kuliko inavyosifiwa sasa," amesema Kamwe.

"Nina uhakika kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa tunakwenda kushinda mchezo ujao. Mtu akikwambia Mamelodi ina wachezaji wazuri mwambie hata sisi tuna wachezaji bora kuliko wao," amesema Kamwe

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
38m ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
1h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
3h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
9h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE β†’