Katika mkakati wa kujiimarisha kuelekea msimu ujao, Simba imeanza mapema maboresho ya kikosi ikitajwa kumalizana na mlinzi wa kushoto Ibrahim Imoro aliyekuwa akiitumikia Al Hilal ya Sudan
Imoro kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na miamba hao wa soka la Sudan ambao msimu ujao watakuwa sehemu ya timu zitakazoshiriki ligi kuu ya NBC
Mghana huyo mwenye umri wa miaka 24 amewahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji aliyeasisti mabao mengi katika Ligi ya Ghana msimu wa 2021-2022 akitoa pasi tisa, pia ametwaa mataji zaidi ya manne ikiwamo la Ligi Kuu Ghana akiwa na Asante Kotoko msimu wa 2021-2022 na Kombe la Rais (Ghana) 2019 na taji la Sudan Super Cup 2022 akiwa na Al Hilal
Imoro anatarajiwa kutua nchini kabla ya msimu huu kumalizika kujifua na kikosi cha Simba ili aanze kuzoea mazingira ya soka la Tanzania
Tangu avunje mkataba wake na Al Hilal, Imoro amehusishwa na klabu kadhaa hapa nchini zikiwemo Azam Fc na Yanga lakini ni Simba iliyofanikiwa kumuweka katika himaya yake