Yanga - Local

Yanga yaiwinda Mamelodi kimya-kimya

Joel JJ By Joel JJ
25 Mar 2024
Yanga yaiwinda Mamelodi kimya-kimya

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefichua mkakati wa kuiwinda Mamelodi Sundowns kimya-kimya akibainisha kuwa wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanashinda mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ligi ya mabingwa utakaopigwa Jumamosi, March 30

Inafahamika, Mamelodi walituma watu wao mapema kuja kuisoma Yanga jambo ambalo Gamondi na benchi lake la ufundi walilibaini na hivyo kubadili mbinu za maandalizi kuelekea mchezo huo

Yanga kwa sasa inafanya maandalizi yake katika uwanja wa Bandari na sio Avic Town ambako ndiko iliko kambi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara

"Sisi hatujalala tupo kazini, tunafahamu kila kitu kuhusu Mamelodi Sundowns, tumeamua kwenda kupambana nao kimya kimya"

"Kila kitu kuhusu ufundi wao wakiwa ugenini tayari tunavyo muda mrefu tukiendelea kuvifanyia kazi. Bahati kubwa kwetu ni kwamba tuna benchi la ufundi ambalo mbali na kuijua Mamelodi pia tumefanikiwa kupata Kila taarifa zao ambazo zitatusaidia kutimiza mipango yetu ya kupata ushindi"

"Tunachokiomba tu ni wachezaji wetu kurejea wakiwa salama kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, tumeacha wao waseme mitandaoni, hatujatoka mchezoni kama ambavyo watu wanavyoichukulia hii mechi, tunawaheshimi Mamelodi lakini dakika 90 za nyumbani tunapaswa kuonyesha ukubwa wetu," alisema Gamondi

Mkakati wa 'kuwapoteza maboya' Mamelodi ulianza tangu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold, Mamelodi watarajie kukutana na Yanga iliyokamili siku ya Jumamosi

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
13m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
27m ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
1h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
1h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
2h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
14h ago
READ MORE →