Wachezaji Thomas Ulimwengu wa Singida Fountain Gate na Erasto Nyoni wa Namungo Fc wamefutiwa kadi nyekundu walizopewa katika mchezo uliozikutanisha timu hizo katika Ligi Kuu Bara ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ikielezwa kwamba zilitolewa kimakos
Ulimwengu na Nyoni walionyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo ambapo timu Singida iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kadi nyekundu zilitolewa tatu, huku mbili zikifutwa
Katika mchezo huo wachezaji walioonyeshwa kadi ni Nyoni (Namungo), Dickson Ambundo (Singida Fountain Gate) na Ulimwengu. Taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa leo imeeleza kuwa imefuta kadi za Ulimwengu na Nyoni baada ya kujiridhisha kupitia picha jongeo
"Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta kadi nyekundu walizoonyeshwa wachezaji Thomas Ulimwengu wa Singida Fountain Gate na Erasto Nyoni wa Namungo FC baada ya kujiridhisha kupitia Ushahidi wa picha jongeo na taarifa za wakufunzi wa waamuzi kuwa hawakustahili adhabu hiyo kwa kosa walilotenda," imesema taarifa hiyo.