Simba - Local

Benchikha aipania Al Ahly

Joel JJ By Joel JJ
28 Mar 2024
Benchikha aipania Al Ahly

Kocha Mkuu wa Simba Abdelhak Benchikha amesema yeye na wachezaji wake hakuna jambo wanafikiria zaidi ya kupata ushindi dhidi ya Al Ahly na kutinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Kesho Ijumaa Simba itakuwa mwenyeji wa Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali CAF CL ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 3 usiku

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Benchikha amesema hakuna jambo lisilowezekana, wanayo nafasi ya kupata ushindi dhidi ya Al Ahly na kutinga nusu fainali

Benchikha amewataka mashabiki wa Simba kuwa na imani na timu yao, wajitokeze kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa hapo kesho

"Nataka kuivusha Simba Robo fainali na kwenda Nusu fainali, hayo ni malengo yangu hadi wachezaji, nataka tuende mbele zaidi tofauti na ambapo Simba huwa inafikia"

"safari hii nataka kuivusha Simba na najua wachezaji wangu wapo tayari. Hakuna kitu kigumu katika mpira, sisi Simba tunaenda kupigana kwenye hatua hii kuanzia nyumbani hadi ugenini"

"Kikubwa mashabiki wetu kuwa na imani na sisi na kujitokeza kwa wingi uwanjani kuwaunga mkono wachezaji katika mchezo huu muhimu," alisema Benchikha

More Stories

Yanga yapambana kuondoa kadi nyekundu ya Aziz Ki kabla ya derby ya simba
Yanga yapambana kuondoa kadi nyekundu ya Aziz Ki kabla ya derby ya simba
1h ago
READ MORE →
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
19h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
20h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
22h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
22h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
23h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
23h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1d ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1d ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1d ago
READ MORE →