Simba - Local

Miquissone mambo magumu Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Apr 2024
Miquissone mambo magumu Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Luís Miquissone leo anatimiza siku 264 tangu alipojiunga tena na Simba akitokea Al Ahly Julai 22/2023.

Miquisson aliondoka nchini msimu wa 2020/21 akiwa amefanya mambo makubwa ndani ya kikosi cha Simba ikiwa ni pamoja na kutwaa taji la Ligi Kuu Bara, lakini tangu amerudi mambo yake ni magumu.

289; Ni dakika alizocheza tangu aliporudi kwenye mechi 15 za ligi huku timu yake ikiwa imecheza mechi 19, hivyo amekosekana kwenye michezo minne.

Miquissone amecheza mechi dhidi ya Mtibwa Sugar akitumika dakika 18 timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 4-3, alipata nafasi tena kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union akicheza dakika 58 Simba ilishinda 3-0, kisha alicheza dakika mbili dhidi ya Mashujaa timu yake ikishinda 2-0.

Pia alipata nafasi ya kucheza dhidi ya Dodoma Jiji ugenini akitumika kwa dakika 23 timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0, akapewa dakika 90 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Coastal Union wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Miquissone alicheza dakika tisa (9) kwenye mechi dhidi ya Singida Fountain Gate wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1, alipata nafasi nyingine dhidi ya Mashujaa akitumika kwa dakika 10 Simba wakishinda bao 1-0, dhidi ya Ihefu FC alicheza dakika 29 Simba walishinda 2-1.

Mechi nyingine alizocheza ilikuwa ni dhidi ya Yanga akitumika kwa dakika 16, Simba wakipoteza kwa mabao 5-1, alipangwa tena dhidi ya Namungo akicheza dakika (16) Simba akiambulia sare ya bao 1-1, dhidi ya Tabora Unitedi alicheza dakika moja na walishinda 4-0, dhidi ya Azam FC alicheza dakika 13 wakiambulia sare ya bao 1-1.

Dhidi ya Geita Gold alicheza dakika nane wakishinda bao 1-0 ugenini, na mechi dhidi ya KMC alicheza dakika moja Simba wakitoka sare ya mabao 2-2 na mchezo mwingine ni dhidi ya JKT Tanzania pia aliitumika dakika moja na timu take ikishinda bao 1-0.

Ukweli ni kuwa yule Miquissone mwenye kasi ya haraka na uamuzi mzuri akiwa nje au ndani ya 18 bado anajitafuta.

Simba ikiwa imetupia mabao 39 katika mechi 19 walizocheza hadi sasa katoa pasi tatu za mabao na mechi zote waliambulia pointi tatu.

Dhidi ya Mtibwa Sugar alimpa Clatous Chama ikiwa ni pasi yake ya kwanza, Singida Foutain Gate na Ihefu alitoa pasi mojamoja mtupiaji akiwa ni Moses Phiri.

Hana bahati chini ya makocha wote wawili waliomfundisha tangu amerejea ndani ya kikosi cha Simba akianza na Roberto Oliveira 'Robertinho' alishindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Hadi ameondoka hakuwahi kumpa mchezo hata mmoja kuanza na kauli yake dhidi yake ilikuwa ni kumpa muda zaidi ili kupunguza kiro.

Chini ya kocha wa sasa anayeinoa Simba, Abdelhak Benchikha amepata nafasi ya kuanza kwenye mchezo mmoja tu akitumika kwa dakika zote 90 dhidi ya Coastal Union wakishinda mabao 2-1

Mwanaspoti

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’