Simba imedondosha alama mbili Ruangwa baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Wily Onana aliitanguliza Simba kwa bao la shuti kali nje ya 18 lakini Namungo Fc wakasawazisha kabla ya mapumziko kupitia Kelvin Sabato
Edwin Balua akafunga bao maridhawa kupitia mpira wa adhabu katika dakika ya 69 lakini dakika za majeruhi Namungo wakarejea mchezoni kwa bao la kujifunga beki wa Simba Kennedy Juma
Hakukuwa na mawasiliano kati ya Kennedy na mlinda lango Ayoub Lakred katika kucheza mpira uliopigwa na Meddie Kagere ambao haukuwa ukionekana kuwa na madhara
Simba imeendelea kupoteza matumaini katika mbio za ubingwa na pengine sasa itakuwa na kazi ya kuchuana na Azam Fc kuwania nafasi ya pili ili kujihakikishia tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao